Lectio Divina

Fr. Richard Rohr, OFM | Jumamosi, 1 Februari 2025

Lectio divina, (kwa Kilatini: “usomaji mtakatifu”) ni njia ya kutafakari maandiko kwa upendo, utulivu, na sala ya kina. Katika lectio divina, Mungu hutufundisha kusikiliza na kumtafuta katika kimya.

“Mkristo aliyekomaa humwona Kristo katika kila kitu na kila mtu mwingine.”[1]

Hatua za Lectio Divina:

        1.  Usomaji wa Kwanza

Ruhusu nafsi yako itulie na uanze kujizoeza na maneno. Soma andiko hilo kwa sauti, polepole na kwa uwazi. Simama kwa muda mfupi wa pumzi moja au mbili kabla ya kuendelea.

        2.  Usomaji wa Pili

Sikiliza kwa moyo ulio tulivu, uliyo katikati, na angalia ni neno au kifungu gani kinajitokeza kwako au kinakugusa kwa namna ya kipekee.

        3.  Usomaji wa Tatu

Baada ya kimya cha muda mfupi, soma andiko tena kwa mara ya tatu. Tafakari jinsi neno au kifungu hicho kinahusiana na hali yako ya sasa kimaisha. Kaa na neno hilo au kifungu hicho kwa dakika moja, ukizingatia hadi kihusiane na mwili wako, moyo wako, na ufahamu wako wa ulimwengu unaoonekana na usioonekana. Unaweza kutamka majibu yako kwa sauti au kuyaandika kwenye daftari lako la kutafakari.

       4.  Usomaji wa Mwisho

Jibu kwa sala au maelezo ya kile ulichokipitia. Mwalike Mungu mwenye hekima isiyo na mipaka akuongoze katika maeneo yenye kutatanisha, yasiyojulikana, au yaliyojaa tamaa au tumaini.

 

Zoezi la Kutaamuli Kimya Kimya (Contemplative Sit):

Ukianza na nukuu hii hapa chini, fanya kikao cha kimya kwa kutafakari. Unaweza kuweka muda kwa kutumia saa au kengele ya sala kwa dakika 5, 10, au 20 ili ujue muda wa kumaliza.

Kaa sehemu tulivu. Baada ya kutulia, soma tena kwa sauti:

“Mkristo aliyekomaa humwona Kristo katika kila kitu na kila mtu mwingine.”

  • Tambua kama kuna msongo au mkazo kwenye mabega au shingo yako, na ruhusu misuli yako ilegee.
  • Ruhusu mgongo wako upumzike katika nafasi ya kawaida, isiyoegemea sana.
  • Jikita ardhini na ruhusu pumzi yako itulie. Kisha sema kwa sauti:

 

Sijaribu “kufanikisha” chochote. (Pumzika)

 

Hakuna malengo. (Pumzika)

 

Ninakuwa na ufahamu wa wakati huu. (Pumzika)

 

Ninagundua uwepo wangu katika sasa. (Pumzika)

 

Ninapotambua mawazo, hukumu, maamuzi, au wazo lolote linalonijia, naliruhusu lipite kwa sasa. (Pumzika)

 

Badala yake, nazingatia uzoefu wa sasa wa kuwa katika uwepo wa Mungu. (Pumzika)

 

Uwepo wa Mungu. (Pumzika)

 

Uwanja mkubwa zaidi. (Pumzika)

 

Katika Kristo (En Cristo). (Pumzika)

 

  • Piga kengele ya sala kuashiria kwamba kikao cha kutafakari kimya kimenza.

 

Rejea

Richard Rohr, The Universal Christ: How a Forgotten Reality Can Change Everything We See, Hope For, and Believe (Convergent: 2019), 33.

Richard Rohr, The Universal Christ: Companion Guide for Groups (CAC Publishing: 2019), 23–24, 25, 172.

(Vitabu vyote viwili vimenukuliwa katika Tafakari, Daily Meditations, cac.org)

 

 

 


[1] Richard Rohr, The Universal Christ: How a Forgotten Reality Can Change Everything We See, Hope For, and Believe (Convergent: 2019), 33.

⟵ Rudi kwenye Orodha